Chama cha Wanahabari wa kike nchini AMWIK kimesema kuna haja ya wanahabari wa kike kuhamasishwa kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuwaepusha na dhulma wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.
Kulingana na afisa anayehudumu katika chama hicho Bernard Ogoi hatua hii itapunguza visa vinavyoshuhudiwa vya wanawake kudhulumiwa kingono kupitia mitandao ya kijamii.
Ogoi amefichua kuwa AMWIK imeanzisha hamasa maalum kwa wanahabari wa kike kuhusu jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kwa njia inayofaa.
Hata hivyo ameitaka serikali kutolegeza kamba katika vita dhidi ya utumizi mbaya wa mitandao akihimiza kuadhibiwa vikali kwa wanaotumia mitandao ya kijamii kwa namna zizisostahili.
Taarifa na Hussein Mdune.