Story by: Gabriel Mwaganjoni
Jumla ya familia 5 katika eneo la Bondora gatuzi dogo la Rabai kaunti ya Kilifi zimenufaika na ufadhili wa kimasomo kwa watoto wao waliomaliza darasa la nane mwaka wa 2022.
Licha ya watoto hao kupata alama 350 na zaidi katika mtihani wa kitaifa wa KCPE mwaka wa 2022, walikuwa bado hawajajiunga na kidato cha kwanza kutokana na ukosefu wa karo.
Mmoja wa wazazi wa watoto hao Gladys Dama ameeleza mahangaiko aliyoyapitia kabla ya kampuni ya Simba Cement kujitolea na kuwalipia karo watoto hao.
Wakati uo huo, Msimamizi wa kampuni ya Devki Peter Paul ambaye ni mmiliki wa kiwanda hicho cha kutengeneza simiti cha Simba amesema mbali na ufadhili wa karo kampuni hiyo itawekeza katika kuwapatia chakula cha msaada wakaazi wanaoishi katika mazingira duni.