Jumla ya Wanafunzi 25 wa chuo cha TUM mjini Mombasa waliyotiwa mbaroni mapema leo baada ya kushiriki maandamano wamewachiliwa huru hivi punde bila kufunguliwa mashtaka yeyote.
Afisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Makupa Mohammed Osman amesema hatua hiyo imeafikiwa ili kuwawezesha Wanafunzi hao kurudi shule na kuendelea na masomo yao,akioanya kwamba iwapo hawatadumisha utulivu watatiwa nguvuni tena na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Wanafunzi hao wameshiriki maandamano mapema hii leo wakilalamikia mtaala mpya wa masomo katika chuo hicho na kwamba unawakandamiza sawa na kuwapotezea muda.
Wakiongozwa na Gilbert Wafula wanafunzi hao wameutaka usimamizi wa chuo hicho kurudisha mfumo wa elimu wa zamani wakidai kwamba mfumo huo una afuani kwa wanafunzi.