Story by Hussein Mdune-
Baadhi ya shule kutoka kaunti ya Kwale zimefanya vyema katika mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE huku shule ya msingi ya kibinafsi ya Mumtaz mwanafunzi wa kwanza akiwa ni Changoma Idd aliyepata alama 404.
Changoma Idd ambaye ni mwnafunzi wa kwanza shuleni humo amelezea furaha yake huku mwalimu mkuu wa shule hiyo Oliver Wafula akisema ni kupitia juhudi za wazazi na walimu ndio kumefanikisha matokeo bora.
Katika shule ya msingi ya Samburu mwanafunzi wa kwanza ni Leah Nadzua Tsimba aliyepata alama 397, Yusufu Kombo Juma akiwa wa pili kwa 381 na watatu akiwa Sofia Chari Jira aliyepata alama 372.
Hata hivyo Mwalimu mkuu wa shule hiyo Mgunya Mganga amewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanajiunga na shule za upili.
Hata hivyo shule ya msingi ya kibinafsi ya Muungano iliyoko Samburu wanafunzi wa kwanza ni Bilal Athman aliyepata alama 385, Joyleen Wakio akipata alama 384, Brian Maundu akipata alama 381 huku Mwalimu mkuu wa shule hiyo Alex Kombo akisema licha ya sehemu hiyo kukubwa na kiangazi juhudi za wazazi na walimu zimefanikisha matokeo hayo.