Story by Mwanaamina Fakii –
Maafisa wa afya ya jamii katika gatuzi dogo la Matuga kaunti ya Kwale wameshirikiana na mabalozi wa hedhi salama na kutoa hamasa kuhusu umuhimu wa hedhi salama kwa wanafunzi walio na changamoto za kiakili mjini Kwale.
Akizungumza baada ya kupeana mafunzo hayo, Balozi wa hedhi salama Kasisi Francis Mgalla amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa wanafunzi hao hasa wakike.
Kiongozi huyo wa kidini amesema ni vyema iwapo wanafunzi wote wavulana na wasichana wataelimishwa kuhusu umuhimu wa hedhi salama kwani hatua hiyo itapunguza unyanyapaa kwa wasichana shuleni.
Hata hivyo mpango huo wa mafunzo kuhusu hedhi salama umewanufaisha zaidi ya wanafunzi 100 sawia na kuzikabili changamoto mbalimbali zinazowasibu.