Story by Hussein Mdune
Shirika linaloshughulikia maswala ya kutoa mafunzo kwa vijana la CAP Youth Empowerment ikiwamo maswala ya kilimo limewahimiza wazazi ambao watoto wao hawajafanya vyema kwenye mitihani ya kitaifa kujiunga na vyuo vya kiufundi.
Kulingana na afisa wa shirika hilo Francis Emajong, hatua ya wazazi kutowapeleka watoto wao ambao hawajafaulu kumechangia vijana wengi kupitia maisha magumu.
Francis amesema ni jukumu la wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata masomo ya ujuzi,akiitaja hatua hiyo kama njia moja wapo ya kubuni ajira.
Hata hivyo amesema hatua hiyo itawafanya vijana wengi kukabiliana na kupanda kwa gharama ya maisha na hata kujitenga na makundi ya kihalifu na utumizi wa mihadharati.