![](https://radiokaya.co.ke/wp-content/uploads/2020/01/TANDAZA.jpg)
Zaidi ya wanafunzi 76 kutoka eneo bunge la Matuga wamepata ufadhili wa Karo na Pamoja na vifaa mbalimbali vya kimasomo kupitia mradi wa wakfu wa Tandzaza.
Tandaza amesema kuwa hatua hiyo ni njia moja wapo ya kuinua viwango vya elimu katika kaunti ya kwale .
Mbunge huyo aidha amesema kuwa zoezi hilo ambalo limegharimu takribani shilingi laki tatu limelenga zaidi familia ambazo hazijiwezi ikizinagtiwa kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaokosa kupata masomo bora wanatoka kwa familia hizo kutokana na kutokuwa na uwezo huku akiwataka wanafunzi kutia bidii katika masomo yao.
kwa upandewao wazazi ambao watoto wao wamenufaika na zoezi hilo wamelitaja zoezi hilo kama lenye manufaa katika kuimarisha maisha ya wanafunzi.
Baadhi ya vifaa ambavyo wamenufaika kwenye zoezi hilo nipamoja na vitabu vya kusoma ,vitabu vya kuandika ,sare miongoni mwa vinginevyo.