Picha kwa hisani –
Wanafunzi 68 na waalimu watano wa shule ya upili ya wasichana ya Bahati huko Nakuru wamethibitishwa kupata maambukizi ya virusi vya Corona.
Akithibitisha maambukizi hayo hii leo waziri wa afya katika serikali ya kaunti ya Nakuru Kariuki Gichuki amesema wagonjwa hao kwa sasa wametengwa huku wanafunzi wengine 115 wa shule hio wakiekwa karantini ya lazima.
Gichuki amesema jopo maalum la wahudumu wa afya limepewa jukumu la kuwapa matibabu wanafunzi na waalimu wa shule hio walioambukizwa virusi hivyo vya corona ili kuhakikisha afya yao inaimarika.
Waziri huyo ametoa hakikisho kwamba wizara ya afya ya kaunti hio inachunguza maambukizi ya virusi vya corona katika kaunti nzima ya Nakuru sawa na katika taasisi zote za elimu katika kaunti hio.