Picha kwa hisani –
Wanafunzi 38 wa shule ya upili ya marafa katika kaunti ya Kilifi wamethibitishwa kupata mamabukizi ya virusi vya corona.
Gavana wa Kilifi Amason Jeffa Kingi amesema wanafunzi hao walioambukizwa corona wametengwa ndani ya shule hio na kwamba serikali ya kaunti hio itawapa chakula na huduma za matibabu kipindi chote watakapokua karantini.
Kingi amewasihi wakaazi wa kaunti hio kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara ya afya ya kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo,akieleza hofu kwamba maambukzii yanaongezeka kwa kasi ndani ya kaunti hio.
Itakumbukwa kwamba hapo jana gavana kingi alitishia kufunga baadhi ya shughuli katika kaunti hio iwapo wakaazi wataendelea kupuuza maagizo ya kukwepa mamabukizi.