Aliyekuwa Seneta wa Machakos Johnstone Muthama sasa amekihama rasmi chama cha WIPER juma moja tu baada ya kuandikiwa barau kufika mbele ya kamati ya nidhamu ya chama hicho kujitetea.
Muthama amesema anaunga mkono azma ya Naibu Rais Dkt William Ruto ya kuwa rais wa taifa hili akisema hajutii kubanduliwa katika chama cha WIPER kwani chama hicho alikihama tangu mwaka wa 2017.
Akizungumzia kauli hiyo ya Muthama, Mwenyekiti wa chama cha WIPER Balozi Charau Ali Mwakwere, amesema Muthama bado yuko ndani ya Wiper kwani jina lake bado liko kwenye sajili ya msajili wa vyama vya kisiasa.