Shirika linaloangazia masuala ya amani la Jamii Action Center limewataka wahudumu wa boda boda mjini Kwale kuzingatia sheria za barabarani wanapoendeleza shughuli zao za uchukuzi.
Akizungumza na mwanahabari wetu mkurugenzi wa shirika hilo Omar Challa Athman amesema wanashirikiana na wadau mbali mbali kuhamasisha wahudumu wa boda boda kuhusiana na sheria za trafiki.
Kwa upande wao wahudumu wa bodaboda wakiongzwa na Chiwaya Mwandogo wasema hatua hiyo itachangia kujenga uhusiano mwema kati yao na maafisa wa usalama
Taarifa na Rasi Mangale.