Afisa mkuu wa bodi ya kudhibiti filamu nchini Bonaventure Kioko amesema bodi hiyo imepania kuwadhibu wamiliki wa camera aina ya drone watakao peperusha bila idhini ya bodi hiyo ukanda wa Pwani.
Akiongea mjini Mombasa kioko amesema hatua ya kupeperusha kamera hizo bila idhini na vibali hitajika kumechangia kishuhudiwa visa vya magaidi kuvamia sehemu mbalimbali kwani wanatumia kusoma ramani ya sehemu kwa kutumia kamera hizo.
Hata hivyo amesema kuwa yoyote atakayepatikana akipeperusha kamera hizo bila vibali hitajika kutoka kwa bodi hiyo basi watachukuliwa hatua Kali za kisheria.
Hata hivyo amesema itasaidia kuimarisha usalama zaidi huku akihimiza idara ya usalama kushirikiana na bodi hiyo kuwakabili watakao kiuka agizo hilo.
Taarifa na Hussein Mdune.