Taarifa na Charo Banda.
Serikali ya kaunti ya Kilifi yawatengea eneo mbadala wafanyibiashara walibomolewa vibanda vyao mjini Malindi ili waendelea na biashara zao.
Mwakilishi wa wadi ya Shela Kadenge Mwathethe amesema wafanyibiashara hao ambao walikuwa wakiendesha shughuli zao mkabala mwa hospitali ya Malindi walivunjiwa vibanda vyao kutokana na athari za kiusalama katika eneo hilo.
Kadenge amehoji kuwa kabla ya serikali ya kaunti hiyo kuchukua hatua ya kuvibomoa vibanda hivyo, kumeshughudiwa visa kadhaa vya utovu wa usalama vilivyosababishwa na waraibu wa dawa za kulevya.
Aidha amewataka wafanyibiashara hao kuwa makini na kutoruhusu wahalifu kuvitumia vibanda vyao kama maficho, akiwasisitiza kuripoti kwa polisi washukiwa wa uhalifu.