Story by Gabriel Mwaganjoni–
Wagombea wa ubunge wa Nyali walioshindwa katika kinyang’anyiro cha ubunge katika cha uchaguzi wa Agosti 9, kwa kauli moja wameoukosoa uchaguzi huo wakidai ulikumbwa na udanganyifu.
Wakiongozwa na Said Abdhalla maarufu Saidoo wameapa kuwasilisha kesi Mahakamani kupinga matokeo hayo yaliyotangazwa na tume ya IEBC kutokana na utata ulioshuhudiwa katika uchaguzi huo.
Akizungumza na Wanahabari, Abdhallah amesema licha ya wagombea hao kuripoti malalamishi yao kwa maafisa wa IEBC hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Ni kauli iliyoungwa mkono na muaniaji mwengine wa ubunge wa eneo hilo kwa tiketi ya chama cha Wiper Millicent Odhiambo aliyesema kutoruhusishwa kwa baadhi ya mawakala wao katika vituo vya kupigia kura inadhihirisho wazi kwamba kulikuwa na njama fiche.
Hayo yakijiri tume ya IEBC imemtangaza Mohammed Ali wa chama cha UDA kuwa mshindi wa ubunge wa eneo la Nyali baada ya kujizolea jumla ya kura elfu 32,988 huku mpinzani wake wa karibu Said Abdallah akipata kura elfu 18,642.