Picha Kwa Hisani –
Rais Uhuru Kenyatta ameagiza kuchunguzwa kwa sakata ya ufujaji wa fedha katika taasisi ya usambazaji dawa nchini KEMSA na ripoti kuhusiana na sakata hiyo kuwekwa wazi kwa umma katika muda wa siku 21.
Akitoa agizo hilo kutoka Ikulu ya Nairobi wakati wa kulihutubia taifa, Rais Kenyatta ameitaka idara ya upelelezi wa jinai nchini DCI na Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC kuchunguza tuhma hizo na wahusika kuchukuliwa hatua.
Kiongozi wa nchi, amesema juhudi hizo zinafaa kutekelezwa kwa haki na uwazi ili kuvifaidi vizazi vijavyo katika msingi unaofaa na kuliboresha taifa hili kiuchumi na maendeleo.
Wakati uo huo, Kiongozi wa nchi amemuagiza Waziri wa Afya nchini pamoja na na Mwenyekiti wa baraza la Magavana nchini kushirikiana wanaibuka na mikakati itakayohakikisha juhudi za kukabiliana na Corona zinaekezwa zaidi.
Hata hivyo ameongeza muda wa kafyu kwa siku 30 zaidi kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi alfajiri na vilabu vya usiku na baa vikiendelea kufungwa kwa siku 30 zaidi huku akiongeza idadi ya watu wanaofaa kuhudhuria mazishi na harusi kutoka watu 15 hadi 100 pekee.