Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amesema ni lazima wasimamizi wa kampuni za ulinzi za kibinafsi kuwakagua kwa kina walinzi wao kabla ya kuwaajiri katika kampuni hizo.
Hii ni baada ya kubainika wazi kwamba baadhi ya walinzi wa kibinfasi katika eneo la Pwani wamekuwa wakishirikiana na mtandao wa majambazi na kutekeleza uhalifu katika biashara na makaazi mbalimbali katika ukanda huu.
Akizungumza baada ya kufanya mkao wa kiusalama na wamiliki wa kampuni za kibinafsi za ulinzi katika ukanda wa Pwani, Elungata amewataka walinzi hao kuwafichua wahalifu hasa walanguzi wa mihadarati.
Kwa upande wake, Mmiliki wa kampuni ya kibinafsi ya ulinzi ya Winster humu nchini Antony Ndegwa amesema juhudi hizo zimeimarishwa ili kuwakabili walinzi wa kibinafsi wanaoshiriki uhalifu.