Story by Mercy Tumaini –
Walimu wawili wa shule ya upili ya wavulana ya St. Georges eneo la Kaloleni katika kaunti ya Kilifi wamefikishwa katika Mahakama ya Mariakani kwa kosa la uchochezi.
Joaninah Wangeci Kabugu na mwenzake Nicholas Ouma Gor wanadaiwa kutoa matamshi hayo mnamo tarehe 20 na 21 mwezi Oktoba mwaka huu hali ambayo yalichangia vurugu katika shule hiyo na kuchangia shule hiyo kufungwa.
Wakiwa mbele ya Hakimu Stephen Ngii, wawili hao wamekana mashtaka dhidi yao na wakaachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 50 ama pesa taslimu shilingi elfu 20.
Kesi hiyo itatajwa mnamo tarehe moja mwezi Disemba mwaka huu.