Picha kwa hisani –
Walimu wa madrassa katika Kaunti ya Mombasa wameihimiza Serikali kufungua shule hizo, ili kuwawezesha walimu hao kupata mapato.
Wakiongozwa na Ustadh Khamis Mwinyi kutoka eneo la Magogoni huko Kisauni, Walimu hao wa kidini wanasema kwamba wametaabika mno kutokana na ukosefu wa kipato, kwani tegemeo lao kuu lilikuwa ada chache wanazotoa wazazi wa Wanafunzi katika shule hizo.
Akizungumza huko Kisauni hii leo, Mwinyi amesema japo kuna mikakati ya kufungua upya shughuli za masomo kwa wanafunzi, shule hizo za madrassa zimesahaulika katika mchakato huo.
Kulingana na Mwinyi, hali ya maisha ya Walimu hao kwa sasa ni ya kusikitisha akiyasihi Mashirika ya kidini kuwakimu walimu hao kwa mahitaji msingi wakati huu wa janga la virusi vya Corona.