Watu 9 wanaotoka katika jamii inayoishi na uwezo maalum kule Kinango kaunti ya Kwale wamefaidika na vifaa mbalimbali ikiwemo mashine za kushonea nguo, kuchomelea vyuma na Useremala.
Ufadhili huyo kutoka kwa Shirika la kitaifa linashuhulika na walemavu la National Funds for disabled Kenya, limesema vifaa hivyo vitawasaidia kujikimu kimaisha.
Akiongea wakati wa kupeana vifaa hivyo Mwenyekiti wa Shirika hilo Profesa Julia Ojiambo amesema engo kuu la Shirika hilo ni kuwawezesha wanajamii hao wenye mahitaji maalum kujisaidia maishani.
Ojiambo amewataka wanajamii wanaoishi na watu wenye uwezo maalum kujitokeza na kuwasajili watu hao kupata vifaa kwa niaba yao ila akawasihi wasimamizi hao kuwa waaminifu. Agnes Nadzuwa mmoja waliofaidika na vifaa hivyo amelipongeza Shirika hilo kwa kuwatambua watu wanashi na uwezo maalum.
Taarifa na Mariam Gao.