Baraza la kimataifa linaloshughulika na maswala ya walemavu nchini tawi la Mombasa limesema limesajili zaidi ya watu 4,000 wanaoishi na ulemavu katika kaunti hiyo mwanzoni mwa mwaka huu.
kulingana na afisa anayehudumu kwenye baraza hilo Juliet Ruwa hatua hiyo imetokana na ongezeko la walemavu katika kaunti hiyo huku akisema idadi hiyo ya usajili ingali bado ni ndogo mno hivyo basi akazitaka familia zinazoishi na watoto walemavu kujitokeza.
Aidha ameyataka mashirika yanayoshughulika na maswala ya walemavu kushirikiana vyema na serikali katika kuhamasisha jamii mashinani kama njia moja wapo ya kukabiliana na changamoto za walemavu.
Hata hivyo amesema kuwa kama baraza wanapania kuanzisha mradi maalum wa kuyasajili mashirika ambayo yanahusika na maswala ya ulemavu kama njia moja wapo ya kurahisisha utendakazi wao.
Taarifa na Hussein Mdune.