Mkurugenzi idara ya utabiri wa hali ya anga kaunti ya kilifi, Ramadhan Munga amehimiza wakulima kuutumia vyema msimu wa mvua chache ili kuweza kupata mavuno.
Munga amesema kuanzia mwezi wa sita, saba na hadi wa nane huwa ni msimu wa mvua chache ambayo ikitumiwa vizuri huenda mkulima akafaidika kutokana na mvua hiyo.
Ramadhan amesema kuwa mvua hiyo hufanikisha zaidi mimea ambayo haihitaji mvua nyingi mmoja wao ukiwa mmea wa mtikiti.
Munga aidha amsema kuwa maeneo ya Mtwapa na Mida ni sehemu ambazo zimepata mvua nyingi katika msimu huu kutokana na wingi wa miti huku maeneo ya Bamba, Midoina na sehemu zingine zisizokuwa na miti mingi zikikosa mvua hii.
Munga amewahimiza wakazi wa sehemu hizo kuendelea kupanda miti kwa wingi ili kuvutia mvua ya msimu huu.