Mtaalam na mkaguzi wa masuala ya Kilimo Japhet Muthoka, amesema wakulima wa kaunti ya Kwale wanafaa kupanda mimea ambayo inaweza kukua na kuvunwa kwa mda mfupi wakati huu wa msimu wa mvua fupi.
Muthoka amesema katika shughuli za upanzi wa Mahindi, itakuwa bora zaidi endapo wakulima watanunua na kupanda mbegu ya DHA4 ambayo huchukua miezi miwili kukua.
Muthoka ametaja kuwa mbali na mmea wa Mahindi, wakulima pia wanafaa kuzingatia Kilimo cha pojo na kunde, kwani mimea hiyo huchukua mda mfupi na pia huhimili kiangazi.
Aidha amesema mmea wa kunde unafanya vizuri zaidi katika kaunti ya Kwale na pia gharama yake ya kuikuza iko chini.
Taarifa na Mariam Gao.