Mwakilishi wa wadi ya Mwereni eneo bunge la Lunga Lunga kaunti ya Kwale Manza Beja amewataka wakulima katika eneo hilo kukumbatia mbinu za kilimo za kisasa wakati huu wanapoendeleza upanzi katika mashamba yao.
Akizungumza na mwanahabari wetu Beja amesema kuwa mara nyingi wakazi wa eneo hilo ukumbwa na baa la njaa kwani wengi wao upata mazao haba kwa kutumia mbinu duni za kilimo.
Wakati huo huo Manza amesema uchimbaji wa bwawa la Mwakangala litasaidia pakumbwa wakaazi wa eneo hilo kuendeleza kilimo nyunyuzi.
Wadi ya Mwereni ni kati ya maeneo ya kaunti ya Kwale yanayokumbwa mara kwa mara na baa la njaa.
Taarifa na Rasi Mangale.