Story by Hussein Mdune-
Wakulima kutoka wadi ya Mwavumbo gatuzi dogo la Kinango kaunti ya Kwale wameiomba serikaki na wafadhili mbalimbali kuwasaidia na vifaa vya kisasa ili kuendeleza kilimo biashara.
Wakiongozwa na Mbeyu Murira ambaye anajihusisha na kilimo cha Mahindi, Pojo na Kunde katika eneo hilo amesema idadi kubwa ya wakulima wanaendeleza shughuli za kilimo karibu na mito hali ambayo ni changamoto kwao.
Wakulima hao wamesema mvua zinaponyesha maji hubakia kwenye mito bila kutumika, akihoji kwamba iwapo watapata vifaa hivyo basi itasaidia kupata mavuno bora.
Wakati uo huo wamewataka wakaazi wa kaunti ya Kwale kujihusisha na shughuli za kilimo ili kuzalisha chakula kwa wingi.