Story by Hussein Mdune –
Katibu katika Wizara ya Kilimo nchini Prof Hamad Boga amewahimiza wakulima katika kaunti ya Kwale kuiweka mimea yao kwenye Bima kupitia mradi wa kitaifa wa KCEP CRAL.
Akihutubia wakulima wa kaunti ya Kwale katika hafla ya kutoa malipo ya bima kwa wakulima hao, Prof Boga amesema hatua hiyo itasaidia wakulima kuepuka hasara wanazopata pindi mimea yao inapoathirika na kiangazi.
Boga hata hivyo ameweka wazi kwamba tayari wakulima 13,523 kutoka kaunti ya Kwale, Kilifi na Taita Taveta ambao wako kwenye mradi huo wa kitaifa wa KCEP CRAL ambao mimiea yao iliathirika na kiangazi watafidiwa.
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo na ufugaji katika serikali ya kaunti ya Kwale Joan Nyamaso amesema shilingi milioni 13 zitafidiwa wakulima 2,954 kutoka kaunti ya Kwale ambao mimea yao iliathirika na kiangazi.