Story by Mwahoka Mtsumi –
Wakili na mchanganuzi wa maswala ya kisiasa George Kithi amedai kuwa atawasilisha kesi Mahakamani kusisitiza kusitishwa kwa baadhi ya sheria kandamizi za uvuvi zinazoshinikizwa na Mamlaka ya ubahari nchini KMA na wadau wengine.
Kithi ameilaumu Mamlaka hiyo kwa kutowahusisha wavuvi katika utungaji na utumizi wa sheria hizo kama vile ada ya laki moja ya leseni kwa manahodha wa maboti ya wauvuvi.
Akizungumza katika kaunti ya Kilifi, Kithi amesema sheria hizo zinafaa kupigwa msasa kwani zimekuwa zikiwandamizi wavuvi kwa miaka mingi licha ya wavuvi hao kutegemea shughuli za uvuvi katika kujipatia mapato.
Kwa upande wao wavuvi katika ufuo wa bahari hindi wa eneo la Shela mjini Malindi wakiongozwa na Salim Ali Mohamed wamelalamikia usumbufu kutoka kwa askari wanaosimamia usalama wa baharini nchini.