Baadhi ya Wanasheria kutoka eneo la Pwani wametishia kuelekea Mahakamani kupinga hatua ya Mamlaka ya Kilimo na Chakula nchini AFA kwa kusambaza mbegu za mkorosho katika kaunti ya Makueni badala ya eneo la Pwani.
Wanasheria hao wakiongozwa na Wakili George Kithi wamesema hatua hiyo itawakandamiza wakulima wa Pwani ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakiendeleza kilimo cha mkorosho.
Wakili Kithi amesema hatua ya Mamlaka hiyo kusambaza mbegu hizo za mkorosho kaunti ya Makueni ni ishara wazi kwamba serikali imelitenga eneo la Pwani katika kilimo cha mkorosho
Wakili Kithi amesisitiza kwamba ni lazima mamlaka hiyo kushuritishwa ili kulitambua eneo la Pwani kama kitovu cha zao la mkorosho sawia na kukiboresha zaidi kilimo hicho kwani kaunti ya Kilifi ndio yenye kampuni ya korosho.
Kauli ya wanasheria hao imejiri baada ya Afisa wa mbegu na mimea ya mafuta katika Mamlaka hiyo Florence Kubai kuzindua rasmi usambazaji wa mbegu za mkorosho katika kaunti ya Makueni, Embu na Tharaka Nithi.