Baada ya timu ya soka ya Harambee Stars kuandikisha matokeo duni mbele ya Senegali kwenye mechi ya kundi C ya mchuano wa kuwania kombe la mataifa ya bara Afrika (AFCON) sababu mbali mbali zimetolewa kuhusu matokeo hayo.
Wakenya wengi wamelaumu wachezaji lakini hata hivyo kuna wale ambao wameona kuwa kifo cha Bob Collymore ndio sababu ya kushindwa.
Wakenya wanaamini kuwa kwa sababu ya kuomboleza kwao basi Senegali wamepata urahisi wa kuwashinda.
Tazama baadhi ya mambo yaliyoandikwa mtandaoni hapa chini: