Story by Janet Shume-
Maafisa wa idara ya upelelezi wa jinai nchini DCI wamewakamata wanaume watatu wenye umri wa makamo waliopatikana na myamapori aina ya Pangolin pasi na vibali vyovyote kwa idara ya KWS katika eneo la Kinango kaunti ya Kwale.
Watatu hao wamekamatwa baada ya maafisa hao kupokea ripoti kutoka kwa wakaazi wa eneo hilo.
Akithibitisha suala hilo, Afisa mkuu wa Shirika la uhifadhi wa wanyamapori nchini KWS tawi la kaunti ya Kwale Jacob Orahle amewaonya vikali wale wanaoendeleza biashara ya uwindaji haramu, akisema hawatasazwa na mkono wa sheria.
Hata hivyo Shirika la kijamii la Justice Restoration and Child Care JURECCO kupitia Mwenyekiti wake Mohammed Mwakulaya limelalamikia utendakazi duni wa Shirika la KWS kaunti ya Kwale, akisema KWS imeshindwa kuwajibikia majukumu yake.
Watatu hao waliotiwa nguvuni na mnyamapori huyo ni pamoja Pas Mwita wa umri wa miaka 30, Kabwere Tembe wa miaka 26 na Salim Nduria wa umri wa 22.