Story by Mwahoka Mtsumi –
Wataalam wa kiafya humu nchini wamesema huenda wakenya wakajipata pabaya baada ya kushuhudia dalili za kuwepo kwa wimbi la nne la virusi vya Corona nchini.
Wataalam hao wa kiafya wakiongozwa na Daktari Martin Kuria wamesema kutokana na kuripotiwa kwa aina mpya ya virusi vya Corona kutoka nchini India na Afrika kusini ni lazima wakenya wawe waangalifu.
Daktari Kuria amesema tayari baadhi ya wakenya wamepatikana na virusi hivyo huku akiwataka wananchi kuwa waangalifu zaidi hasa kwa kuzingatia kanunu za Wizara ya afya nchini ikiwemo kuvaa barakoa.
Wakati uo huo Wizara ya afya nchini imezindua awamu ya pili ya kutoa dozi ya chanjo ya Corona kwa wakenya ambao tayari wamepokea dozi mara ya kwanza.