Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta hapo kesho siku ya Jumanne anatarajiwa kuwaongoza wakenya katika sherehe za Mashujaa Day, sherehe ambazo zimepangwa kufanyika katika kaunti ya Kisii.
Kiongozi wa nchi, anatarajiwa kuandamana na Naibu Dkt William Ruto katika sherehe hizo ambapo wakenya watakuwa wakiadhimisha sherehe hizo za miaka 57 tangu taifa lijinyakulie uhuru.
Sherehe hizo za Mashujaa zitaandaliwa katika uwanja wa Gusii kule kaunti ya Kisii huku watu zaidi ya elfu nne wakitarajiwa kuhudhuria sherehe hizo kwani wakuu wa maandalizi hayo, wakiongozwa na Katibu katika Wizara ya usalama wa ndani Dkt Kiranja Kibicho wakisema maandalizi hayo yamekamilika.
Hata hivyo sherehe hizo pia zimepangwa kuandaliwa katika kaunti mbalimbali nchini hapo kesho, ambapo Kaunti ya Kwale itaandaa sherehe hizo katika uwanja wa shule ya msingi ya Lungalunga, Mombasa katika bustani ya Mama Ngina na kaunti ya Kilifi katika uwanja wa chuo kikuu cha Pwani.