Picha kwa hisani –
Askofu mkuu wa Kanisa katoliki jimbo kuu la Mombasa Martin Kivuva amewahimiza wakaazi wa Ukanda wa Pwani kutopuuza masharti ya kiafya ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
Askofu Kivuva aliyekuwa akizungumza katika makaazi yake rasmi kule Nyali kaunti ya Mombasa amesema janga la Corona limewaangamiza watu wengi ikiwemo Viongozi wa kidini nchini, ni lazima wakenya kuwa waangalifu.
Kiongozi huyo wa kidini amewataka wakaazi wa Ukanda wa Pwani kuzingatia masharti yote ili kuukwepa ugonjwa huo.
Wakati uo huo, ameitaka Serikali kutoifanyia mzaha sekta ya afya na badala yake kuafikiana na wahudumu wa afya ili kuzuia migomo ya mara kwa mara ya wahudumu wa afya nchini.