Story by Hussein Mdune-
Huku Kenya ikitarajiwa kujiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya kimataifa ya mazingira dunia tarehe 5 mwezi Juni, Shirika la huduma kwa wanyamapori nchini KWS limeonya kuwachukulia hatua za kisheria wakaazi wanaoharibu mazingira.
Kulingana na Naibu Afisa msimamizi wa mbuga ya wanyamapori ya Shimba Hills kaunti ya Kwale Gilbert Njeru, kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiingia kwenye mbuga hiyo na kukata miti kiholela.
Njeru amesema Shirika hilo limepiga marufuku watu kuingia katika mbuga hiyo na kuharibu raslimali, akihoji kwamba kuna hatari kubwa ya binadamu kuvamiwa na wanyamapori.
Hata hivyo amewahimiza wakaazi wa kaunti ya Kwale kulinda mazingira kwa kupanda miti kwa wingi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.