Story by Mwanaamina Fakii:
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata, amewataka wananchi ambao hawajajisajili kama wapiga kura kujitokeza na kufanya hivyo kabla Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kukamilisha zoezi hilo.
Akizungumza na Wanahabari katika kaunti ya Kwale, Elungata amewataka wakaazi ambao hawana vitambulisho vya kitaifa kutembelea afisi za idara ya usajali wa watu ili kupata vitambulisho hivyo na kushiriki katika zoezi la usajili wa wapiga kura.
Elungata amehoji kwamba tume ya IEBC haitaongeza mda mwengine baada ya zoezi hilo kukamilika huku akiwataka wananchi kutumia fursa iliyopo kujisajili.
Wakati uo huo amevitaka vitengo vya usalama kuwa makini zaidi katika jukumu la la kuimarisha usalama ili kuhakikisha visa vya utovu wa usalama havishuhudiwa wakati wa uchaguzi.