Story by Hussein Mdune-
Huku kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais ikitarajiwa kuanza rasmi siku ya Jumanne baadhi ya viongozi wa kidini mjini Mombasa wamewataka wakenya kuipa nafasi Mahakama hiyo kutekeleza jukumu lake.
Wakiongozwa na Askofu wa kanisa la ushindi Baptism eneo la Likoni Joseph Maisha, viongozi hao wamesema Mahakama ni taasisi huru hivyo basi haipaswi kuingiliwa utendakazi wake.
Kiongozi huyo wa kidini amewataka wakenya kuwa na subra mpaka pale Mahakama itakapotoa uamuzi wake kuhusiana na kesi hiyo huku akiwasihi viongozi wa kisiasa kudumisha amani.
Wakati uo huo amewataka wakaazi wa kaunti ya Mombasa kudumisha amani wakati zoezi la uchaguzi wa ugavana huku akiwasihi kumchagua kiongozi atakayechangia maendeleo mashinani.