Story by Our Correspondents-
Kenya inajiunga na mataifa mengine Ulimwenguni unaadhimisha siku ya kimataifa ya Afya ya akili duniani.
Siku hii inaadhimishwa katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwahamisha wananchi kuhusu umuhimu wa afya ya akili, utetezi dhidi ya unyanyapaa wa jamii sawa na kuwawezesha wananchi kuwasaidia wale wanaopitia changamoto za afya ya akili.
Shirika la Afya duniani WHO iliidhinisha siku hii ramsi mwaka 1992 kwa lengo la kuhakikisha nchi wanachama zaidi ya 150 wanakumbatia juhudi za kuzikabili changamoto za afya ya Akili.
Hata hivyo nchini Kenya, wadau mbalimbali wa maswala ya afya kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii, wamechukua jukumu la kuwahamisha wananchi kuhusu jinsi ya kuepuka changamoto za afya ya akili.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni Make Mental and Wellness for All a Global Priority.