Picha kwa Hisani –
Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i ametangaza kuwa tarehe 10 mwezi Oktoba mwaka huu yani hapo kesho, itakua sikukuu ya kitaifa ya huduma yaani Huduma Day.
Katika taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari na kutiwa saini na Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i, imesema wakati wa siku hiyo wakenya watashiriki maombi kwa taifa hili sawa na kutekeleza huduma za kujitolea katika jamii.
Waziri Matiang’i vile vile amewataka wakenya kukumbatia maombi, sawa na kuimarisha umoja na mshikamano katika jamii zao kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
Haya yanajiri huku taifa likiwa limeanza rasmi siku tatu za maombi ya kitaifa.