Picha kwa hisani –
Serikali ya kitaifa imezindua rasmi zoezi la kutoa kadi za huduma namba kwa wakenya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo katika kaunti ya Machakos,waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia Joe Mucheru amesema ugavi wa kadi za huduma namba utaanza rasmi tarehe moja mwezi ujao wa disemba
Mucheru aidha amefichua kwamba ifikapo tarehe 12 mwezi disemba mwaka ujao wa 2021, vitambulisho vya sasa vya kitaifa havitatumika tena na kwamba ni kadi za huduma pekee zitakazotumika.
Kwa upande wake waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i amesema ni wakenya milioni 37 pekee walisajiliwa kwenu mpango huo,akisema watahakikisha wakenya wote wanasajiliwa ili wapate huduma kwa urahisi.
Matiang’i aidha amesema kadi za huduma zitasaidia pakubwa kumaliza ufisadi sawa na kuhangaishwa kwa wananchi wanaotafuta huduma katika afisi za serikali.