Wakazi wa eneo la Sabaki huko Magarini kaunti ya Kilifi, wanaitaka serikali kuingilia kati na kusuluhisha utata unaozunguka shamba la kilimo la ADC eneo hilo.
Wakiongozwa na mwakilishi wa wadi ya Sabaki eneo hilo Edward Kazungu Dele, wakaazi hao kwa kauli moja wamesema kuwa endapo serikali haitawajibikia suala hilo miradi wa kilimo na ufugaji iliyoathirika tangu kuanza kwa mzozo huo itazidi kuathirika.
Wakaazi hao wamezidi kudai kwamba shamba hilo kwa sasa linauzwa kwa watu binafsi na usimamizi wa ADC huku agizo la rais mstafu Mwai Kibaki kuwa wenyeji wapewe takriban ekari 950 likikosa kutekelezwa kufikia sasa.
Kwa sasa wanatoa mwito kwa katibu msimamizi katika wizara ya ardhi Gideon Mung,aro kuingilia kati na kuhakikisha wakaazi wanatendewa haki.
Taarifa na Esther Mwagandi.