Takriban wakazi 300 ambao hujihusisha na shughuli za ukulima eneo Madunguni wadi ya Kakuyuni sasa wanakila sababu ya kutabasamu baada ya kupokea vifaa vya ukulima kutoka kwa serikali ya kaunti ya Kilifi.
Vifaa hivyo ikiwemo majenereta na mabomba ya maji vimeigharimu serikali ya kaunti ya Kilifi takriban shilingi milioni nane kutoka kwa hazina ya maendeleo ya wadi kaunti ya Kilifi.
Kulingana na mmoja wa wakazi waliobahatika kupokea vifaa hivyo Bahati Taura ujio wa vifaa hivyo utasadia pakubwa kufufua kilimo chao ambacho kilikua kimepotea kufuatia mafuriko yaliyoshuhudiwa hivi majuzi.
Taarifa na Charo Banda.