Wakazi wa Bamba kaunti ndogo ya Ganze wameandamana kupinga uuzaji wa ardhi ya ranchi ya Giriama.
Wakiongozwa na mbunge wa Ganze Teddy Mwambire wakaazi hao wameitaka serikali kuingilia kati na kuzuia uuzaji wa ardhi hiyo yenye ekari 66.
Akizungumza na wanahabari wakati wa maandamano hayo mmoja wa wakaazi William Fondo ameitaka serikali kufutilia mbali mikataba yote iliyowekwa na kuregesha shamba hilo kwa wenyeji.
Naye mbunge wa eneo hilo Teddy Mwambire amesema kwamba ataelekea mahakamani kupinga uuzaji wa ardhi hiyo.
Mwambire amedai kuwa wakurugenzi wa ranchi hiyo pamoja na kampuni inayodaiwa kuuza ardhi hiyo wanafanya hivyo kwa manufaa yao binafsi.
Taarifa na Marieta Anzazi.