Picha kwa hisani –
Wakazi wa magarini Kaunti ya kilifi sasa wameelezea hofu yao kutokana na nzige ambao wamezagaa katika eneo hilo.
Kulingana na wakaazi wa eneo hilo wadudu hao wameonekana katika maeneo mbali mbali japo hawajafanya uharibifu wowote hadi sasa.
Wakiongozwa na Joshua Chome wakaazi hao wanaitaka serikali kufanya kila juhudi kukabiliana na wadudu hao kabla uharibifu wa mimea kufanywa.
Wakaazi hao wa Mtsangamali ambao wanategemea kilimo kiuchumi, wanasema wanahofia kuwa huenda wakakumbwa na baa la njaa iwapo serikali itawaachilia nzige hao kufanya uharibifu katika mashamba yao.
Lakini kulingana na waziri wa Kilimo kaunti ya Kilifi Luciana Sanzua tayari ametuma maafisa wake eneo hilo kutathimini hali halisi ili hatua za dharura zichukuliwe mara moja.