Wakazi wa kijiji cha Mwatundo eneo la Kikambala wameandamana kupinga ujenzi wa ukuta kwenye ardhi ya ekari 35 ambayo wanaizozonia baina yao na bwenyenye mmoja.
Akizungumza na wanahabari kwa niaba ya wakazi hao Wisdom Mwalimu amesema kuwa ujenzi huo ni kinyume na sheria kwani mzozo huo uko kotini ukisubiri uamuzi.
Wisdom ameitaka serikali ya Kitaifa kuingilia kati ili kusitisha unyakuzi wa ardhi ambao umekithiri mkoani Pwani
Kulingana na Esha Baya ni kuwa familia ardhi hiyo ni ya mababu zao na haoni sababu ya mabwenyenye kuja kuwanyanyasa kwani wameishi hapo kwa miaka mingi.
Hali hiyo inajiri huku eneo la Kikambala likiendelea kukumbwa na mizozo mingi ya ardhi huku wenyeji wakilalamikia viongozi wa utawala kwa kuchangia hali hiyo.
Taarifa na Maritta Anzazi.