Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta, amedokeza kuwa wakati umefika sasa kwa jamii zengine pia kushikilia nafasi ya urais wa taifa hili ifikapo uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Kiongozi wa nchi, amewataka wakenya kuondoa taswira kwamba taifa hili huongozwa na jamii mbili pekee, akisema nafasi ya urais haijazuiliwa mtu yeyote yule wa taifa hili kuipigania.
Rais Kenyatta amesema kila mkenya ana nafasi na uwezo wa kuliongoza taifa hili kwa kuzingatia katiba ya nchi na udemokrasia, sawia na kuwaelekeza wakenya malengo na mipango atakayoifanywa iwapo wakenya watamchagua.
Wakati uo huo amehimiza mshikamano wa wakenya, kwa kuhakikisha wanaendeleza umoja wa taifa, amani na upendo sawia na kujitenga na siasa za vurugu ambazo huenda zikaligawanya taifa hili.