Wakazi wa eneo la Lango Baya kaunti ndogo ya Malindi kaunti ya Kilifi wanakila kila sababu ya kutabasamu baada ya barabara ya lami inayounganisha Baolala hadi kivuko Baricho eneo la Lango Baya kukamilika.
Wakazi hao wakiongozwa na Balozi wa nchini Tanzania Dan Kazungu wanasema mradi huo wa barabara kutoka serikali kuu utafungua eneo hilo la Langobaya kibiashara na miundo msingi ili maisha ya wakazi waliokuwa wakitaabika yaweze kuboreshwa.
Aidha Kazungu vile vie amesema kuwa serikali vile vile inalenga kuanzisha miradi ya viwanda vya matunda na mboga ili kutenga nafasi za ajira kwa vijana sawia na wakazi wa kaunti ya Kilifi kwa jumla.
Lilian kadzo mmoja wa wakazi hao wanasema kuwa ilikua wakitabika hata Zaidi pindi wanapohitaji huduma hasa za afya katika eneo la Malindi kutokana na usafiri duni.