Story by Gabriel Mwaganjoni
Waqfu wa Shariff Nassir umezindua zoezi la kuwasaidia wakaazi wa kaunti ya Mombasa kwa chakula hususan waathiriwa wa mvua.
Mmoja wa wale walionufaika na msaada huo ni Mwanajuma Mwatsahu mkaazi wa eneo la Ziwani Lasco mjini Mombasa aliyeeleza jinsi mafuriko hayo yalivyowaathiri wakaazi hao.
Mwanajuma aliyekuwa akizungumza na Wanahabari amesema mvua hiyo imepelekea maji taka kutapakaa ndani ya nyumba zao hali inayohofiwa kwamba huenda ikachangia mkurupuko wa maradhi ikiwemo kipindupindu.
Hata hivyo, wakaazi hao wanaiomba Serikali ya kaunti ya Mombasa kuwapatia makao mbadala kwani nyumba zao zimefurika maji.