Wakaazi wa kaunti ya Kwale wamehimizwa kuzingatia vyakula vya lishe bora ikiwemo mboga na matunda ili kujenga kinga zaidi ya mwili.
Kulingana na Mtaalam wa Lishe kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu, Caren Tamiru, wengi wa wakaazi wamekuwa wakila vyakula vinavyotokana na ngano, akisema kaunti ya Kwale ina ardhi yenye rutuba kwa wakaazi kufanya kilimo cha mboga.
Caren amesema kila mmoja ana jukumu la kuzingatia vyakula vya lishe bora hasa vyakula kama matunda na mboga, akihoji kwamba hatua hiyo husaidia kuimarisha kinga ya mwili.
Wakati uo huo amewataka wakaazi kulichukulia kwa uzito swala la lishe bora, akisema hatua hiyo itaimarisha kinga bora ya mwili.