
Story by Hussein Mdune-
Mgombea wa kiti cha ubunge wa Likoni Hamis Domoko amewahimiza wakaazi wa eneo hilo kujitenga na viongozi wenye nia ya kuwagawanya katika misingi ya dini na ukabila.
Akiwahutubia wakaazi wa Likoni, Domoko amesema wakati umefika sasa kwa wakaazi wa Likoni kuwachagua viongozi wenye maono ya maendeleo na ambao watajali maslahi yao.
Amewataka wakaazi wa Likoni na kaunti ya Mombasa kwa jumla kutokubali kutumiwa vibaya na badala yake kuwachagua viongozi kwa misingi ya sera za maendeleo.