Story by Ephie Harusi –
Mkurugenzi wa idara ya hali ya anga kaunti ya Kilifi Getrude Leshamta amewataka wakaazi kupanda miti kwa wingi katika mashamba yao ili kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi.
Kulingana na Leshamta, hali ya mabadiliko ya tabia nchi yamechangiwa pakubwa na ongezeko la hewa kaa inayotokana na ukataji wa miti kiholela na viwanda huku akidai kwamba hali hiyo imeathiri pakubwa sekta ya Kilimo na uvuvi.
Akizungumza na Wanahabari, Leshamta amesema ni lazima wakaazi wazingatia utunzaji wa mazingira iwapo wanalenga kukabiliana na makali ya kiangazi na kuzalisha chakula.
Kwa upande wake Mtafiti wa Mazingira na hali ya bahari hususan nyasi za bahari katika Shirika la Wildlife Conservation Society Alpheen Mbodze ameunga mkono kauli hiyo akisema uharibifu wa mazingira umechangia kupungua kwa uzalishaji wa samaki baharini.