Story by Hussein Mdune
Naibu msaidizi wa Kamishna katika eneo la Kasemeni kaunti ya Kwale Peter Sironga Ole masaa amesema mabadiliko ya tabia nchi yamechangiwa na wakaazi katika eneo hilo kujihusisha na ukataji wa miti ovyo.
Ole masaa amesema swala la ukame katika eneo hilo na kaunti ya Kwale kwa ujumla litamalizika endapo wakaazi watapanda miti kwa wingi.
Aidha amesema kama maafisa wa serikali wameanza kutoa hamasa kwa wakaazi kuhusu jinsi ya kutambua umuhimu wa kupanda miti.
Wakati uo huo amesema kama viongozi wa usalama watahakikisha wanawachukukilia hatua kali za kisheria wanao jihusisha na ukataji wa miti kiholela.